Sisi HakiRasilimali-PWYP, jukwaa la Asasi za Kijamii ambazo zinashughulikia masuala ya madini, mafuta na gesi nchini Tanzania, tumefuatilia kwa umakini miswada mipya ya madini iliyosomwa kwa mara ya kwanza bungeni tarehe 29 Juni 2017.

Miswada iliyosomwa kwa mara ya kwanza bungeni hapo ni:

  1. Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.
  2. Muswada wa Sheria ya Mamalaka ya nchi kuhusu Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017.
  3. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2017
  4. Read more: PRESS RELEASE-MISWADA2017