October 26, 2021

Asasi za Kiraia zinazofanya shughuli za kimkakati kwenye Sekta mbalimbali nchini Tanzania zimeeleza kuridhishwa na namna ambavyo imeshirikishwa na Serikali wakati wa zoezi la uandaaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo (FYDP III 2020/21 – 2025/26. Reynald Maeda kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzan.....

AZAKI: Tumeshirikishwa Kikamilifu Kuandaa Mpango wa Tatu wa Maendeleo
Asasi za Kiraia zinazofanya shughuli za kimkakati kwenye Sekta mbalimbali nchini Tanzania zimeeleza kuridhishwa na namna ambavyo imeshirikishwa na Serikali wakati wa zoezi la uandaaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo (FYDP III 2020/21 – 2025/26.

Reynald Maeda kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) alithibitisha hili wakati akichangia mdahalo kuhusu FYDP III uliofanyika Jumatatu Oktoba 25, 2021 katika Ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma, Tanzania.

Alisema hii ni mara ya kwanza kwa Serikali kuzishirikisha Sekta Binafsi na Azaki wakati wa uaandaaji wa mpango huu muhimu wa kitaifa wa maendeleo, na kuongeza kwamba hatua hiyo itasaidia kuongeza ushiriki wao kwenye hatua ya utekelezaji wa mpango huo ambao ulizinduliwa nchini mwaka huu.

Maeda ambaye alikuwa ni miongoni wa wazungumzaji wakuu wakati wa mdahalo akiwa kama mwakilishi wa Asasi za Kiraia nchini ambapo aliwataka Azaki nchini kutokuwa na hofu yoyote juu ya ushiriki wao kwenye uaandaji na utekelezaji wa FYDP III.

“Moja ya maeneo ambayo tumeshiriki wakati wa uaandaaji wa mpango huu ni pamoja na kuingiza Takwimu zilizozalishwa na Asasi za kiraia kwenye Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuhusu utekelezaji na ufuatiliaji wa mpango,” alisema Maeda.

Related Posts

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 02, 2025

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

ESKi Tanzania ni programu ya kukuza uwezo iliyoundwa ili kukuza na kuendeleza kizazi kipya cha viongozi, watetezi wa jamii na wataalamu wanaoshughulik...

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 01, 2025

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

Capacity-building opportunity for CSOs, youth and media to deepen technical expertise.

External audit services tender
Aug 14, 2025

External audit services tender

HakiRasilimali invites qualified firms to submit proposals for annual audit engagements.