November 06, 2024

DODOMA: Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini imeshauri wadau katika sekta ya uziduaji kufikiria teknolojia mpya itakayowawezesha wachimbaji wadogo kuepukana na matumizi ya zebaki katika uchimbaji wa dhahabu. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Ma...

"Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Yashauri Teknolojia Mpya kwa Wachimbaji Wadogo ili kuepuka matumizi ya zebaki, kulinda afya na kuongeza uzalishaji."
DODOMA: Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini imeshauri wadau katika sekta ya uziduaji kufikiria teknolojia mpya itakayowawezesha wachimbaji wadogo kuepukana na matumizi ya zebaki katika uchimbaji wa dhahabu. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, David Mathayo katika jukwaa la uziduaji 2024 linalofanyika Dodoma tarehe 5 na 6 Novemba, 2024. Jukwaa hilo ambalo limeratibiwa na HakiRasimali na kuzinduliwa na Naibu Waziri Mkuu Dkt.Doto Mashaka Biteko linalenga kujadili na kubadilisha uzoefu miongoni mwa wadau katika sekta ya uziduaji nchini ambayo inajumuisha madini, mafuta na gesi. Mr Mathayo amesema zebaki imekua ikitumika na wachimbaji wadogo katika kuchimba dhahabu kutokana na kukosa njia mbadala jambo ambao limekua likiathiri pakubwa afya za wachimbaji hao.

Amesema matumizi ya teknolojia bora yatawezesha kulinda afya za wachimbaji pamoja na kuongeza uzalishaji. “Hili ni tatizo kubwa ambalo madhara yake kila mmoja anatambua, hata wanaotumia wenyewe wanajua, tunaomba tuendelee kuongeza teknolojia na kuweza kuangalia namna bora zaidi ya kupata dhahabu bila kutumia zebaki,”amesema. Hata hivyo ameiomba serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapa mitaji huku akisisitiza kuwa wachimbaji hao ambao wako kwa asilimia 40 wamekua na mchango mkubwa katika kuongeza pato la taifa. Jukwaa la uziduaji la mwaka huu limeudhuriwa na wadau kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo DRC,Kenya na Uganda.

Related Posts

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 02, 2025

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

ESKi Tanzania ni programu ya kukuza uwezo iliyoundwa ili kukuza na kuendeleza kizazi kipya cha viongozi, watetezi wa jamii na wataalamu wanaoshughulik...

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 01, 2025

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

Capacity-building opportunity for CSOs, youth and media to deepen technical expertise.

External audit services tender
Aug 14, 2025

External audit services tender

HakiRasilimali invites qualified firms to submit proposals for annual audit engagements.