October 28, 2021

Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad amesema kuna haja ya ofisi ya CAG kuwa na wataalamu wabobezi katika sekta ya madini ili kuimarisha ukaguzi katika eneo hilo. Katika mdahalo wa kujadili ripoti ya Shirika la Oxfam ambayo inaangazia nafasi ya wakaguzi wakuu wa S.....

Profesa Assad Azungumzia Umuhimu wa Wataalamu wa Madini, Mafuta na Gesi Ofisi ya CAG
Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad amesema kuna haja ya ofisi ya CAG kuwa na wataalamu wabobezi katika sekta ya madini ili kuimarisha ukaguzi katika eneo hilo.

Katika mdahalo wa kujadili ripoti ya Shirika la Oxfam ambayo inaangazia nafasi ya wakaguzi wakuu wa Serikali katika ukaguzi wa sekta ya madini katika mataifa 10 ya Afrika Profesa Assad amesema kuwa na wataalamu kutaongeza ubora wa ripoti zinazotolewa.

"Wakati mie naondoka ofisini hatukuwa na mjiolojia wala mhandisi wa madini hata mmoja, niliomba mara mbili lakini sikupata," amesema Profesa Assad.

Ameongeza kuwa "Kutokuwa na wataalamu hao ni tatizo kubwa kwa kawaida ilitakiwa walau wawepo wanajiolojia watano, Wahandisi watano. na wataalamu wa mafuta na gesi watano bila kuwa na wataalamu hao katika ukaguzi ni tatizo kubwa"

Related Posts

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 02, 2025

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

ESKi Tanzania ni programu ya kukuza uwezo iliyoundwa ili kukuza na kuendeleza kizazi kipya cha viongozi, watetezi wa jamii na wataalamu wanaoshughulik...

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 01, 2025

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

Capacity-building opportunity for CSOs, youth and media to deepen technical expertise.

External audit services tender
Aug 14, 2025

External audit services tender

HakiRasilimali invites qualified firms to submit proposals for annual audit engagements.