Na Marco Maduhu (ESKi Tanzania Alumni)

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojariwa utajiri wa Rasilimali Madini, Gesi asilia na Mafuta. Utajiri huu ni kinyume na maisha halisi ya wananchi wake.

Rais wa kwanza wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania – Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliweka Dira ya Rasilimali kuwa madini yanufaishe watanzania kwanza kupitia Azimio la Arusha. Hivyo, rasilimali zote zilizokuwa zinamilikiwa na watu binafsi hususani wageni zilirudishwa chini ya umiliki wa umma wa watanzania, na serikali ikiwa muangalizi mkuu.

Kutokana na changamoto za ujuzi, kukua kwa technolojia pamoja na changamoto za kimitaji mwaka 1997, Serikali ilitunga Sheria ya Madini kukaribisha wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza hapa nchini.

Hisia za watanzania waliowengi hususani wanaoishi karibu na maeneo ya uchimbaji ni baada ya kukaribisha wawekezaji miaka ya 1990, rasilimali zetu hususani Madini, mafuta na gesi asilia hazinufaisha tena watanzania zaidi ya kunufaisha nchi/makampuni yaliyowekeza hapa nchini.

Mwaka 2010 Serikali ilifanya tena marekebisho ya sheria ya madini na kuweka masharti kwa wawekezaji, kuwa ajira, utoaji wa huduma mbalimbali ndani ya migodi wapewe kipaumbele wazawa (Local Content), pamoja na kuwajibika kwenye Jamii kwa kushirikiana na Jamii kuhusika kujandaa kwa pamoja mipango MADINI HAKIRASILIMALI (Article Maduhu)na kujenga miundombinu ya maendeleo kwenye vijiji/maeneo yanayozunguka migodi (Corporate Social Responsibility).

Soma zaidi:https://www.hakirasilimali.or.tz/wp-content/uploads/2020/10/MADINI-HAKIRASILIMALI-Article-Maduhu-.pdf

 

 

 

 

 

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts

 • 147 words0.7 min read

  HakiRasilimali and Ms Training Centre for Development Cooperation (MSTCDC) are […]

  Read More
 • 89 words0.4 min read

  The 2020 newsletter features mostly HakiRasilimali engagements on COVID19 pandemic: […]

  Read More
 • 259 words1.3 min read

  Being cognizant of the sector’s significance to the country’s economy, […]

  Read More