Serikali inafanya uhamasishaji wa uwekezaji wa viwanda ili Rasilimali zinazopatikana hapa nchini zitumike katika viwanda hivyo kama sehemu ya juhudi za kufungamanisha shughuli za kiuchumi ili kuwa na maendeeo jumuishi.

Hayo yemeelezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe Oktoba 25, 2021 wakati wa mdahalo kuhusu Mpango wa tatu wa maendeleo ya miaka mitano wa mwaka 2021/2021- 2025/2026 na ushamiri wa viwanda vinavyotumia rasilmali asili.

Duniani kote suala sio kuwa na Rasilimali bali Rasilimali hizo zinatumikaje kuleta maendeleo ya watu. Sisi tunaamini kuwa juhudi kubwa zinaweza kufanyika kutumia Rasilimali zilizopo kwa maendeleo ya nchi lakini bila kuwa na viwanda vya ndani vya kutumia Rasilimali hizo tutakuwa bomba la kupitisha faida zilizopo,” amesema.

Amesema Wizara yake kama waratibu wa shughuli za viwanda na biashara wanafanyia kazi suala la kuondoa vikwazo vyote vya uwekezaji kupitia mpango wa Blue Print lakini kuzihuisha sera zate zilizopo chini ya wizara hiyo ili kuendana na mazingira ya sasa na mpango wa maendeleo.

Hivi sasa tunafanya hamasa kwa sekta binafsi za wazawa kuchagamkia fursa zinzojitokeza katika rasilimali zilizopo nchini lakini pia kuhamasisha uwepo wa wazawa wenye utaalamu na ujuzi stahiki ili Watazanzania wengi zaidi waajiriwe huko,” amesema Kigahe.

Aidha ameongeza kuwa kwa sasa Serikali inahamasisha uwekezaji katika viwanda mahususi ambavyo vinatumia Rasilimali zilizopo nchini ili kwanufaisha watanzania walio wengi.