July 11, 2022

Uteuzi wa wajumbe wa Kamati ya TEITA kwa kipindi cha miaka mitatu 2022 -2025 kulingana na mabadiliko ya kifungu cha 5 cha sheria ya TEITI 2015. NaCoNGO kwa kushirikiana na wadau toka Asasi za Kiraia (AZAKI/CSOs) zinazofanya kazi katika sekta ya Madini, Mafuta, na Gesi: Wanatangazia asasi zote zinaz...

Tangazo la Uchaguzi wa Wawakilishi wa AZAKI Kamati ya Taifa ya TEITA
Uteuzi wa wajumbe wa Kamati ya TEITA kwa kipindi cha miaka mitatu 2022 -2025 kulingana na mabadiliko ya kifungu cha 5 cha sheria ya TEITI 2015.

NaCoNGO kwa kushirikiana na wadau toka Asasi za Kiraia (AZAKI/CSOs) zinazofanya kazi katika sekta ya Madini, Mafuta, na Gesi: Wanatangazia asasi zote zinazofanya kazi katika sekta ya Madini, Mafuta, na Gesi kuwa kutakuwa na zoezi la uchaguzi litakalofanyika tarehe 16.07.2022 jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa SeaShells Millenium Hotel kuanzia saa 3 asubuhi.

Tafadhali soma mwongozo wa uchaguzi na fuata maelekezo.

Kila asasi inayotimiza matakwa yaweza kuwa na mgombea mmoja na awasilishe maombi yake kwa anwani ifuatayo: info@nacongo.or.tz.

Maombi hayo yaambatanishwe na vifuatavyo:

Wasifu wa mgombea (CV)
Barua ya maombi ikieleza kifupi kwa nini unafaa kuwa mwakilishi (application letter)
Maelezo ya uwezo wa mgombea yasiyozidi kurasa mbili (personal capacity statement)

Maombi hayo yatumwe kabla ya tarehe 13.07.2022.

Washiriki wote wa uchaguzi wameombwa kujigharamia kufika jijini Dae es Salaam.

Kwa maelezo zaidi piga namba +255 (0) 767 544 560

Chanzo: NaCoNGO Website

Download the Original Document

Related Posts

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 02, 2025

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

ESKi Tanzania ni programu ya kukuza uwezo iliyoundwa ili kukuza na kuendeleza kizazi kipya cha viongozi, watetezi wa jamii na wataalamu wanaoshughulik...

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 01, 2025

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

Capacity-building opportunity for CSOs, youth and media to deepen technical expertise.

External audit services tender
Aug 14, 2025

External audit services tender

HakiRasilimali invites qualified firms to submit proposals for annual audit engagements.