MATARAJIO NA MAPENDEKEZO YA HAKIRASILIMALI-PWYP KUHUSU BAJETI YA WIZARA YA MADINI MWAKA WA FEDHA 2018/19

UTANGULIZI Sekta ya uziduaji (madini, mafuta na gesi asilia) ni kichocheo kwa ukuaji wa uchumi wa nchi. Kwa ukubwa wake, sekta hii inakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi za Kitanzania milioni 4,975,991. Na huchangia asilimia 4.8 ya Pato la Taifa. Kwa sababu hii, sisi HakiRasilimali-PWYP, jukwaa la Asasi za Kiraia linalochambua sera na kufanya uchechemuzi […]