Mchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Abel Kinyondo: “Mabadiliko ya Tabia ya nchi ni tatizo kubwa , Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za kusini mwa jangwa la Sahara zinazoathiriwa na mafuriko” Katika mjadala wa jukwaa la uziduaji linaloendelea jijini Dodoma Profesa Kinyondo amesema Afrika inachangia kiwango kidogo cha hewa lakini inaathirika sawa na mabara mengine.
Amesema tegemeo la rasilimali fedha za kikabiliana na athari zinazojitokeza ni zile za mikopo ambazo badala ya kuleta neeema zinaongeza au kuibua changamoto mpya ya mzigo wa madeni. “Utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa sekta ya uziduaji inaweza kuwa chanzo cha rasilimali za kukabiliana na changamoto hizo wakati ambao Takwimu zinaonyesha asilimia 56 ya hewa chafu yote ilizalishwa na sekta hiyo,” amesema Profesa Kinyondo. Hata hivyo amesema ili kufanikisha hilo zinahitajika jitihada za kudhibiti mianya ya uvujishaji mapato katika sekta hiyo ili mchango wake katika uchumi uwe mkubwa wa kuweza kufadhili shughuli za kukabiliana na changamoto hiyo.

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts