Wadau wa uziduaji wameshauri baadhi ya vipengele vya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 kufanyiwa marekebisho, ili kuongeza ufanisi katika sekta ya madini. Wametoa wito huo leo Novemba 9,2023 katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Uziduaji, lililoandaliwa na Shirikia lisilo la kiserikali la HakiRasilimali, kwa lengo la kujadili mafanikio na changamoto katika sekta ya madini, pamoja na kutoa mapendekezo ya maboresho.
Kwa mujibu wa wadau hao, mojawapo ya kipengele cha sheria ni kile kinacholazimisha makampuni ya uchimbaji madini ya nje kuwa na akaunti ya Benki nchini (Tanzania) tu, hatua inayowakosesha mitaji ya uzalishaji madini. “Uchimbaji madini unahitaji mitaji mkubwa ambayo taasisi zetu za ndani za kifedha bado hazijawa na uwezo wa kukopesha. “Kwa mfano, uzalishaji wa madini ya Nikeli katika mgodi wa Kabanga unahitaji takribani dola za kimarekani billioni moja, kiasi ambacho upatikanaji wake kwa benki za nchini ni changamoto,” amesema Meneja Mkuu wa Kampuni ya Adavale Resources (TZ) Limited, Gerald Mturi. Mwisho

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts