Askofu Mkuu Kanisa la Mennonite nchini, Nelson Kisare, ametoa wito wa sekta ya madini kuzingatia uwazi na uwajibikaji, ili rasilimali za nchi zinufaishe kizazi cha dasa na kijacho. Ametoa wito huo leo Novemba 9, 2023, wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Uziduaji mkoani Dodoma, lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la HakiRasilimali, kwa lengo la kujadili mafanikio na changamoto zilizomomo katika sekta ya madini, pamoja na kupendekeza nini kifanyike kwa maboresho zaidi.
Askofu Kisare amesisitiza kwamba watanzania wanahitaji uziduaji usiochochea ufisadi au rushwa, bali wenye tija,kwa faida ya wananchi na taifa kwa ujumla. “Ipo pia migogoro mingi katika jamii inayotokana na shughuli za uziduaji. Migogoro hiyo iko ndani ya uwezo wetu kuitatua, tuwashirikishe wananchi wenyewe kupata ufumbuzi,” amependekeza, huku akishauri shughuli za uziduaji kuzingatia pia suala la utunzaji mazingira, ili kulinda afya za wanadamu Mwisho

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts