Mwenyekiti wa Bodi ya Hakirasilimali Jimmy Luhende: “Mataifa makubwa duniani yanatusukuma sisi (mataifa yanayoendelea) kwenye nishati safi lakini haimaanishi tukimbilie huko bila kujipanga” Amesema ni muhimu kabla ya kwenda kuhakikisha watu wanajengewa uwezo kupitia njia mbalimbali ikiwemo majukwaa kama haya. “Ni muhimu kuwa na mawazo yetu, maono yetu na muktadha wetu sanjari na kuangalia hata kasi ya kuhamia huko inayotufaa,” amesemq Luhende wakati akitoa neno la ufunzi. Amesema kuhama ni jambo linalohitaji umakini huko akiuliza swali lililoleta mjadala miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo. “Kwanza wanasema tuhame lakini tujiulize tunahama tukitokea wapi, hapa tulipo tumefika kwani,” ameuliza Luhende akimalizia na kicheko kifupi.

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts