Mkurugenzi wa Hakirasilimali Adam Anthony: “Sekta ya uziduaji na nishati ni sekta muhimu kwa Taifa letu. Uhusiano kati ya sekta ya madini na sekta ya nishati hasa katika muktadha wa madini ya kimkakati, nishati mpito na mabadiliko ya tabianchi ni mkubwa sana” Katika jukwa la uziduaji linaloendelea jijini Dodoma Antony amepongeza hatua za kisera za Serikali huku akipendekeza kuimarishwa kwa mazingira rafiki kwa wawekezaji. “Serikali iendelee kuongeza fursa na mitaji ili kuimarisha uwazi katika sekta na kukemea vitendo vya rushwa ili tuweze kufikia Malengo tuliyojiwekea kama Taifa,” amesema. Ameitaja kauli mbiu ya Jukwaa mwaka huu kuwa ni ‘Kufanikisha mhamo wa nishati na maendeleo endelevu katika sekta ya uziduaji Tanzania” Aidha, Jukwaa la Uziduaji mwaka 2023 linaendelea katika hoteli ya Vizano jijini Dodoma likiwa na mada mbalimbali, endelea kufuatilia.

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts